25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Melania Trump mwanamitindo wa kwanza kuingia Ikulu

Melania Trump
Melania Trump

WASHINGTON, Marekani

MKE wa Donald Trump, Melania Trump, anakuwa  mwanamitindo wa kwanza kuingia Ikulu ya Marekani baada ya mume wake jana kuchaguliwa kuwa rais wa nchini hiyo.

Shughuli kubwa ya Melania ni pamoja na kushughulikia masuala yanayohusu ustawi wa jamii na familia kwa ujumla.

Hata hivyo, wajibu huo haujabainishwa kuwa rasmi, lakini mke huyo wa rais anatarajia kuongoza  na kuleta ufanisi katika kampeini mbalimbali zinazohusu nyanja hiyo ya ustawi, kuongoza  shughuli mbalimbali akiwa ikulu na kumwakilisha rais katika masuala mengine.

Mwanamitindo huyo amemtaka mumewe kuacha matumizi ya mitandao wakati  akiwa  na nia  ya  dhati ya kupinga ubaguzi na unyanyasaji  kwenye mitandao.

Melania alizaliwa mwaka 1970 nchini Yugoslavia, pia ni mke wa pili wa rais kuzaliwa nje ya Marekani, baada ya  Lousia Adams, aliyekuwa mke wa  John Quincy Adams, aliyezaliwa  England.

Mwanamitindo huyo aliye na umri wa miaka 46, alianza shughuli za mitindo tangu alipokuwa na umri wa miaka 16  na alipofikisha umri wa miaka 18, alisainiwa na wakala wa shughuli hizo mjini Milan, nchini  Italy.

Picha yake imepamba majarida mbalimbali yakiwemo ya Harper’s Bazaar, Vanity Fair na Jarida la England la GQ.

Mke huyo wa Trump ana miliki kampuni ya vidani na vipodozi mbalimbali na ana uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali ikiwemo Kislovenian, Kiserbia, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani.

Jinsi alivyokutana na mumewe

Mwanamitindo huyo alikutana na Trump katika wiki ya mitindo jijini New York, Septemba mwaka 1998, baada ya kuachana na mkewe wa kwanza Marla Marples.

Walitangaza uchumba mwaka 2004 na kuoana mwaka 2005 jijini Florida nchini Marekani.

Katika harusi hiyo, mke wa Trump alivaa gauni la harusi lililokadiriwa kuwa na thamani ya Dola 100,000, sawa na 213,820,000 za Kitanzania.

Katika harusi hiyo, Hillary na mumewe Bill Clinton walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa na sherehe ilifanyika katika Hotel ya Mar-a-Lago inayomilikiwa na Trump.

Melania alipata haki za kuishi nchini humo mwaka 2001, baada ya miaka 5 na alipata uraia mwaka 2006, mwaka mmoja baada ya kuolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles