24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Mwakamo awatoa hofu wanaume kuhusu mikopo Kibaha

Na Gustafu Haule,Pwani

Mbunge wa Kibaha vijijini, Michael Mwakamo (CCM)amewatoa hofu wanaume wanaolilia fursa ya kupata mikopo kutoka Halmashauri kuwa wawewatulivu kwakuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inalifanyiakazi jambo hilo.

Mwakamo, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 4, mwaka huu katika eneo la Kibondeni lililopo Kata ya Mtongani Kibaha vijijini.

Kauli ya Mwakamo,ilikuja mara baada ya mwananchi mmoja aliyekuwepo katika mkutano huo, Musa Sonyo kuhoji kwanini Wanaume hawapewi nafasi ya kuchukua mikopo katika Halmashauri zao na badala yake wanapewa wanawake, vijana na Walemavu pekee?. 

“Mheshimiwa mbunge naomba kuuliza,hivi kwanini sisi wababa hatupewi mikopo ya Halmashauri wakati mwanamke akikopa tunalipa sisi Wanaume? Mimi naomba na sisi tupewe hiyo mikopo kama wanavyopewa wake zetu ili tuondoe utata katika ndoa zetu,”amesema Sonyo.

Aidha,kufuatia hoja hiyo, Mwakamo amesema kuwa atakwenda kulifanyia utafiti na muda si mrefu wanaume watakuwa katika sehemu ya kupata mikopo kama ilivyo katika makundi mengine.

Mwakamo, ameongeza kuwa kwasasa Halmashauri inatoa mikopo ya asilimia 10 ikiwa asilimia nne kwa Wanawake, asilimia nne kwa Vijana na asilimia mbili kwa Walemavu.

Amesema suala la wababa kupata mikopo lipo na linazungumzwa bungeni na tayari amefanya ziara katika mikoa mbalimbali kupitia kamati yake ya bunge na hoja hiyo aliikuta.

Amesema kulingana na sheria hiyo kwasasa Vijana wanaopewa mikopo vigezo vya umri ni miaka 35 ndio maana wale Wanaume wenye umri wa miaka 45 wanakosa kwa kigezo cha umri.

“Ni kweli mikopo inatolewa lakini Wanaume wenye umri mkubwa wanakosa lakini niwaombe baba zangu tuvute subra kwakuwa Serikali imeliona hilo na  sheria hiyo inafanyiwa kazi na ikikamilika imani yangu mikopo mtapata,”amesema Mwakamo

Aidha, Mwakamo amesema katika kipindi cha miaka miwili alichokaa madarakani Jimbo lake limefanikiwa kupata maendeleo makubwa ikiwemo katika sekta ya elimu na afya.

Amesema,ndani ya muda huo tayari amefanikiwa kujenga Shule za Sekondari tano ikiwemo Kawawa, Disunyara, Bokomnemela, Kikongo na Gwata huku akiahidi kujenga Shule nyingine mwaka huu katika Kata ya Mtongani.

“Nataka niwahakikishie wananchi wangu Shule ya Sekondari Mtongani nitaijenga na matarajio yangu ndani ya miezi mitatu Shule hiyo ianze kujengwa kwakuwa kibali nimepata na ninachosubiri ni kupata wataalamu wa kupima eneo,”amesema Mwakamo.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Mtongani, Habiba Mfaramagoha ,amemshukuru mbunge kwa kufanya ziara katika eneo hilo kwakuwa wananchi wamepata majibu ya kero zao huku akiomba suala la maji na umeme kupewa kipaumbele zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles