25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

MBEYA CITY YATANGAZA KIAMA

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM
BAADA ya kufanikiwa kuondoa gundu la kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu miwili iliyopita, uongozi wa Mbeya City umetamba kuwa kuanzia sasa ni mwendo wa kutoa dozi kwa kila watakayekutana naye.
Mbeya City ilishindwa kuibuka na ushindi katika michezo miwili ya ufunguzi kwa misimu miwili iliyopita, ambapo msimu wa 2015/2016 ilipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar, kabla ya msimu uliopita kuanza kwa suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar.
Lakini msimu huu mambo yanaonekana kuwa mazuri baada ya kikosi hicho kuilaza Majimaji ya Songea mabao 2-0, katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja, alisema usajili walioufanya msimu huu ndiyo unawapa imani ya kurejea makali yao kama ilivyokuwa msimu wa 2013-14 walipopanda daraja kwa mara ya kwanza.
“Tumeanza vizuri msimu huu kwa ushindi dhidi ya Majimaji, haya ni matokeo ya mchanganyiko mzuri wa wachezaji chipuzi na wenye uzoefu, naamini kikosi hiki kitafanya vizuri zaidi ya tulivyofanya tulipopanda daraja kwa kwa mara kwanza,” alisema.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Ndanda FC utakaofanyika Septemba 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, alisema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi makali kuhakikisha kuwa kinaibuka na ushindi ili kuendelea kuvuna pointi tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles