27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

 MAYANGA AKABIDHI MAJUKUMU KWA WACHEZAJI

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga, amesema kwa upande wake amekamilisha maandalizi ya kuikabili Bitswana na sasa amekabidhi majukumu kwa  wachezaji   kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Stars na Bostwana zitavaana kesho katika mchezo wa kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaopigwa kwenye Uwanja Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa takwimu za mara ya mwisho zilizotolewa na Fifa, Tanzania inashika nafasi ya 120 kwa viwango vya ubora wa soka duniani, wakati Bostwana ipo kwenye nafasi ya 140.

Akizungumza na MTANZANIA, Mayanga alisema kikosi chake kimeiva kwa ajili ya Botshwana na kuibuka na ushindi, kwa kuwa amekiandaa kikamilifu baada ya kufanya mazoezi toka Jumatatu ya wiki hii kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

“Tukifanya vizuri tutapanda juu kwenye viwango vya Fifa, hili ni jambo ambalo kila mmoja analitamani, hata mimi mwalimu nitafarijika sana.

 

“Mimi kama kocha nimefanya ninachotakiwa kufanya kuiandaa timu kisha kukabidhi majukumu kwa wachezaji, zaidi ya hapo nawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi Jumamosi waje tushangilie, pia wasisahau kutuombea,” alisema Mayanga.

 

Kikosi cha Botswana kilitarajiwa kuwasili nchini jana  tayari kwa kuivaa Stars kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles