27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kudaiwa kuua mwenzake

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji

Na AMON MTEGA, SONGEA

JESHI la Polisi, Mkoa wa Ruvuma, linamshikilia Yazidu Abina (35), mkazi wa Kijiji cha Mrusha, Wilaya ya Tunduru, mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua Rajabu Mohamed (45) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kichwani na machoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba mbili mwaka huu, usiku katika eneo la Pacha Nne.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwombeji, kabla ya tukio hilo, Rajabu Mohamed alituhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa mtuhumiwa Abina.

“Inasemakana siku ya tukio, mtuhumiwa Abina akiwa shambani, alichukua kitu chenye ncha kali na kumvizia marehemu Rajabu Mohamedi na kumchoma kichwani na machoni kwa kutumia kitu hicho na kumuua,” alisema Kamanda Mwombeji.

Kutokana na tukio hilo, kamanda huyo wa polisi amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kuachana na tabia za kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

“Waambieni wananchi wasiwe na utaratibu wa kujichukulia sheria mkononi kwani huyo aliyemuua mwenzake tutamfikisha mahakamani wakati wowote ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema.

Katika tukio jingine, Kamanda Mwombeji alisema wanawashikilia watu 17 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio mbalimbali ikiwamo wizi wa kuvunja nyumba.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na mali za watu ambazo zilitambuliwa na wamiliki wake baada ya kuwapo kwa taarifa za watu hao kukamatwa.
Alizitaja baadhi ya mali zilizokamatwa kuwa ni compyuta mpakato sita, compyuta za mezani, televisheni 18, redio na vifaa mbalimbali vya pikipiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles