32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

MAUWASA yaendelea na msako wa wezi wa maji mjini Maswa

Na Samwel Mwanga,Maswa

MAMLAKA ya Maji na Usafi na Mazingira mjini Maswa(MAUWASA) iliyoko katika Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imewataka wananchi kujisalimisha kwenye ofisi za mamlaka hiyo ili waweze kuunganishiwa maji kiuhalali na kuacha kuchepusha maji kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Meneja Biashara, Boniface Kasinde(mwenye T-Shirt ya bluu)akiwa na watumishi wengine wa Mauwasa wakiangalia chemba ya Maji iliyoko mjini Maswa iliyohujumiwa na wafanyabiashara wakooshea magari.(Picha Na Samwel Mwanga).

MAUWASA wameendelea na ukaguzi wa miundo mbinu ya maji inayohujumiwa na wananchi wasio waaminifu na kusababisha mamlaka hiyo kupata hasara.

Zoezi hilo limekuwa endelevu kwa wateja wa maeneo yote yanayohudumiwa na Mamlaka hiyo na kufanikiwa kubaini maeneo ya watu mbalimbali wakiwa wanaunganisha maji kwa njia wa wizi.

Matukio ya wizi wa maji yameendelea kuvumbuliwa kwa kasi kubwa ambapo jitihada za Mamlaka zimefanikiwa kuwakata watu mbalimbali wanaohujumu miundo mbinu na kulipa hasara mamlaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 26, baada ya kufanikiwa kugundua wizi wa maji katika maeneo mbalimbali mjini Maswa, Boniface Kasinde ambaye ni Meneja Biashara Mauwasa amesema wameweza kupata taarifa ya wizi wa maji na wamechunguza na kugundua wizi mkubwa unaofanywa kwa kujiunganishia maji nyuma ya mita ya maji.

“Kujiunganishia maji nyuma ya mita ni kosa kisheria unakuwa unahujumu Mamlaka na utakapobainika sheria itachukua mkondo wake maana unakuta mtu amesitishiwa hudumanlakini ndani ya nyumba yake kuna maji.

“Kuna mmoja anfanya biashara ya kuosha magari(Car wash) lakini anatumia maji kwenye chemba ya maji kwa kuchezea miundo mbinu ya maji ya Mamlaka na wanaendelea kupata maji.

“Ni kosa kisheria, na mteja anaunganisha maji nyuma ya mita anakuwa amefanya hujuma na hasara kwa serikali na makosa haya yanapelekea kulipa faini au kufunguliwa kesi na kupelekwa mahakamani na atalipa gharama zote za uharibifu uliofanywa,” amesema Kasinde.

Kasinde amesema miundo mbinu hiyo ni ya muda mrefu na kipindi cha nyuma mita za maji zilikuwa zinafungwa kwa ndani na sasa tumeamua mita zote kuzifunga nje ya uzio wa nyumba.

MAUWASA imeendelea kuwataka wananchi kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji kwani utakapokamatwa sheria itachukua mkondo wake na hakutakuwa na huruma kwa mtu yoyote na faini ni kuanzia Sh 500,000 hadi Sh milioni 10 au kifungo kisichopungua miezi sita hadi Miaka miwili jela au vyote viwili kwa pamoja.

Wateja wa Mauwasa wameombwa kuacha kuchepusha maji na zaidi wajisalimishe kwenye mamlaka ili kuweza kupata huduma ya maji kwa uhalali na kuacha kuhujumu miundi mbinu ya Mamlaka.

Baadhi ya Wateja waliokutwa wakiiba maji ni pamoja na Wateja wa majumbani, wafanyabiashara, taasisi za Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles