31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa walivyoungana kupinga ubaguzi Afrika Kusini

SWAGGAZ RIPOTA

WATU maarufu hawajakaa kimya kufuatia ubaguzi na unyanyasaji wanaofanyiwa raia wa kigeni wanaoishi nchini Afrika  Kusini. Nyota mbalimbali wamepaza sauti zao kukemea vitendo hivyo vinavyohamika kama Xenophobia.

Neno ‘Xenophobia’ ni mchanganyiko wa maneno mawili ya la Kigiriki yaani Xeno lenye maana ya ugeni na Phobia lenye maana ya uoga na yakiungana yanaleta tafsiri ya wenyeji wenye uoga na wageni katika kuzidiwa mali, utajiri, ajira nk.

Sasa Swaggaz tunakupa nukuu za baadhi ya mastaa wa burudani barani Afrika waliopaza sauti zao kupinga na kukemea vitendo hivyo vinavyofanywa na wenyeji wa Afrika Kusini dhidi ya raia wa kigeni.

Tiwa Savage: “Nakataa kuangalia mauaji ya kinyama ya watu wangu Afrika Kusini, hii ni mbaya na kwa sababu hiyo sitatumbuiza kwenye shoo yangu ya Septemba 21, sala zangu ziende kwa wahanga na familia zilizoathirika na hili, kuua mtu yeyote ambaye ni Mwafrika ni mtu wangu iwe ni wa Nigeria au laa.”

WizKid: “Nimesikitishwa sana na baadhi ya maneno ya mastaa, huu siyo muda wa kugombana au kunyoosheana vidole, tuupe upendo nafasi na tutumie akili, watu wanauawa kweli, angalia unachokiongea.”

Fid Q ambaye jana alitakiwa atumbuize Afrika Kusini katika tamasha la MTV Base Show Case Night amesema:“Nimejifikiria kama msanii silioni ‘vibe’ wakati linanitazama kama mgeni ambaye nimeenda kule kuchukua nafasi zao za kazi, ningekuwa kama mtumwa anayekwenda kutumbuiza au kujipendekeza kwa masta wake, siwezi kusema Waafrika Kusini wote ni wabaya, nawafahamu wapo wazuri ambao nawafahamu, nafikiri watu maarufu kukemea hili suala sababu wazee wetu walikuwa wanapigana Afrika iwe moja.”

Nikk wa Pili: “Kinachotokea SA (Afrika Kusini) ni moja ya sifa ya kizazi cha sasa, mihemko pamoja na kuwepo na fursa kubwa ya kujielemisha. Moja ya sifa kubwa ya babu zetu wakati wa utumwa au ukoloni kina Malcom X, Samora, Mwalimu Nyerere ilikuwa ni kujielimisha na kupambana kujifunza. Watumwa Marekani walijifunza wenyewe.”

Skales: “Mnasema wageni wamekuja kuchukua kazi zenu, wanawake wenu, wanaleta uharifu kwenu ila nyinyi ndiyo mnawaua na kuwabaka kila siku,”

Zari The Boss Lady ambaye ni raia wa Uganda mwenye makazi yake jijini Pretoria Afrika Kusini amesema: “Nanyoosha mikono yangu juu, wenyeji wanafanya mambo ya kibaguzi kwa kuwapiga na kuwaibia wageni,”

Rosa Ree: ”Mandela amka uone wanao wanavyofanya kwenye nchi uliyoteseka kuipigania ni muda halali wa Yesu kurudi kutusaidia, eeh Mwenyezi Mungu tusamehe kwani hatujui tuyafanyanyo.”

Lulu: “Afrika tuungane kwa pamoja tukemee ubaguzi huu wanaofanyiwa wageni huko Afrika Kusini.”

Flaviana Matata: “Matukio ya hivi karibuni nchini Afrika Kusini yanaathiri sisi sote kama Waafrika. Matukio ya hivi karibuni yanaathiri sisi sote kama Waafrika, sisi ni ninalaani vikali mashambulio haya ya uhuni na niombe amani katika mitaa ya Afrika na tuone sababu zaidi ya kuwa pamoja sisi ni Afrika.”
 
Burna Boy kupitia akata hili alitofautiana kauli na rapa AKA wa Afrika Kusini aliyeonekana kutopinga vitendo wanavyofanya raia wa nchi hiyo kwa wageni alisema: “Nilikuwa najua hauna akili lakini sikujua kama imefikia huku na tukikutana ni bora uwe na ulinzi mkubwa maana nitakupiga, sijawahi kukanyaga Afrika Kusini toka mwaka 2017 na sasa sitakanyaga tena mpaka vitendo hivyo vya kibaguzi zitakapomalizika.”
Ali Kiba: “Imetosha imetosha, tukatae ubaguzi huu.”
Harmonize: “Hapana hapana, hii kitu haiku sawa, Afrika Kusini dunia inawaangalia, sisi ni wamoja,”
Vanessa Mdee: “Maombi yangu yanaenda kwa kaka na dada zangu wa kigeni wanaoteseka katika makao yao Afrika Kusini. Ni aibu sisi kuchukiana wakati mababu zetu walikufa kwa kuikomboa Afrika Kusini.”
 
Nash Mc: “Katika albumu yangu hii mpya ya Diwani Ya Maalim, kuna wimbo unaitwa Dizonga ni namba 14, nimeongelea mambo mengi sana yanayohusu Afrika Ya Kusini pamoja na Watanzania waishio kule,namshukuru Mungu nimetumia uwezo wangu wa kiuandishi kuuhabarisha umma matukio mbalimbali yanayotokea ulimwenguni, wazulu wanaotumia kigezo cha kukosa ajira kwa sababu ya wageni kutoka nchi zingine za Afrika ambao ni weusi wenzao inaonyesha ni jinsi gani hawataki kutumia nguvu na akili zao walizojaaliwa na Mungu kujitafutia mkate wao wa kila siku.”
Rayvanny ambaye ameamua kutumia ustaa wake kupaza sauti kupitia muziki, alizama studio na kuandika wimbo wenye ujumbe unaosema: “Tazama kinachoendelea usiwe kipofu, fungua macho yako sasa na fikra zako, tuna rangi moja, upendo ndiyo kila kitu tunapaswa kukitafuta sisi ni watoto wa mama Afrika.
“Acha kuichoma na kuiua Afrika, tunahitaji utulivu na siyo dhoruba usitumia bunduki, kisu wala mabomu, ubinadamu unapaswa kuwa kitu tunachomiliki, usiniite mgeni Afrika ni nyumbani, watu wanasema kutembea juu ya maji ni miujiza ila kwangu kutembea kwa amani juu ya dunia ndiyo muujiza wa kweli.”
Peter P Square: “Moyo wangu unasikika huzuni kusikia hadithi za shambulizi huko Afrika Kusini, sisi Waafrika tunapaswa kutafuta njia za maendeleo pamoja kama Waafrika ili kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi kwetu na vizazi vijavyo.”
Yemi Alade: “Imetosha, tutaacha hii iendelee hadi lini? Afrika ndiyo nyumba yetu, tunapaswa kuwa ‘United States of Africa’, hatuhitaji damu hii, tunaweza kufanya vizuri kuliko hii.”
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles