25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Mashindano ya Gofu ya Lina Nkiya kuhamia Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Baada ya Awamu ya kwanza ya Mashindano ya Gofu yaliyofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Gofu, Lina Nkiya kwa kushindana na sasa ni zamu ya Morogoro wanatarajiwa kuchuana kuanzia Aprili 11, 2024.

Michuano hiyo inayoitwa Lina PG Tour imeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) kwa lengo la kumuenzi mchezaji huyo aliyekuwa na mchango mkubwa kwenye timu na TLGU.

Lina alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2011 walipotwaa taji la Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Dar es Salaam.

Makamu Rais wa TLGU, Ayne Magombe amesema mashindano hayo yatafanyika katika mikoa tofauti na hiyo yote ni kuendelea kumuenzi mchezaji huyo kwa kuibua vipaji na kushindana.

“Nategemea kuona ushiriki mkubwa wa wachezaji kama ilivyokuwa Moshi tulipata mwitikio mzuri, hiyo yote tunathamini kile ambacho akifanya Lina enzi za uhai wake alikuwa anapenda sana mchezo huu,”amesema.

Mume wa Lina Said Nkiya amesema sababu ya kuzunguka kufanya utalii wa gofu ni kwa kuwa mke wake huyo aliupenda mchezo huo na kuwasaidia wengi hivyo, wanataka kuendeleza pale walipoishia kwa kusaidia wengine kuinuka.

Amesema kama walivyofanya Moshi kwa kutoa zawadi nzuri wataendeleza kwa watakaofanya vizuri katika mikoa yote watakayoenda na kuwahimiza wachezaji mbalimbali kujitokeza na kujisajili ili kushiriki kwa wingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles