23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘MARUFUKU KUUZA DAWA YA MALARIA’

Editha Karlo, Kigoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepiga marufuku Vituo vya Afya, zahanati na Hospitali za Serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo leo mjini Kigoma wakati alipotembelea Zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma kuangalia hali ya matibabu dhidi ya malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya malaria duniani.

“Nawaagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuweka matangazo yanayoonyesha kipimo cha haraka cha malaria, dawa mseto za kutibu malaria kali ni bure kwenye kila vituo vya kutolea huduma za afya za Serikali.

“Endapo mtoa huduma yeyote atamtoza mwananchi malipo  ya matibabu na vipimo vya malaria hatua stahiki itachukuliwa bila kumuonea huruma,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Ummy amewataka waganga wakuu wa vituo kwa ngazi ya zahanati na waganga wakuu wa wilaya kuweka namba zao za simu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia wananchi kutoa malalamiko yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo hazikidhi viwango ili kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles