Maofisa usalama Marekani wawatimua wahamiaji kwa mabomu

0
814

WASHINGTON, MAREKANI

Maofisa Usalama wa Marekani wawarushia mabomu ya machozi na kuwatawanya wahamiaji waliokuwa wakikaribia kuingia nchini humo kutoka Mexico.

Maofisa wa kulinda mipaka walifunga barabara ambayo ndiyo kivukio kikubwa zaidi cha wahamiaji wanaoingia Marekani katika juhudi za kukabiliana nao.

Hii ni baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba utawala wake hautawaruhusu wahamiaji kuingia Marekani kwa urahisi.

Usafiri ulisitishwa kwa saa kadhaa kufuatia kufungwa kwa barabara kati ya miji ya San Diego na Tijuana, hata hivyo, baadaye shughuli kwenye barabara hiyo ziliruhusiwa kuendelea.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikitanda katika eneo hilo, katika siku za karibuni kufuatia maelfu ya wahamiaji kutoka nchi za Amerika ya Kusini kuwasili kwenye uwanja mmoja wa michezo mjini na Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here