24.3 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mantra Tanzania Limited kusaidia maendeleo Namtumbo

Na Mwandishi Wetu, Namtumbo

Kampuni inayotekeleza mradi wa uchimbaji madini ya‘uranium’ ya Mantra Tanzania Limited,  imeahidi kusaidia maendeleo wilayani  Namtumbo, mkoani Ruvuma kupitia shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa kongamano la Namtumbo Kihenge liloandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya Septemba 21 – 22, 2023.

Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja Uendelevu wa Mradi wa Mantra, Majani Wambura amesema dhamira yao kupitia shughuli za CSR ni kunufaisha jamii kwa muda mrefu pale mradi utakapokamilika.

Ameeleza faida za mradi huo, kuwa ni pamoja na fursa za ajira na biashara mbalimbali  katika  kuendeleza sekta ya madini, huku mkakati wa CSR wa 2023-2028 ukiangazia elimu, afya, uhifadhi wa mazingira na  maendeleo ya jamii.

“Mradi wa Mantra hauhusiani na kuchimba madini ya Uranium pekee bali kuna fursa ambazo zitafaidisha jamii nzima kama vile ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zitakazokuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi.

“Mkakati wetu wa CSR sio tu kurudisha kwa jamii, bali ni kuwezesha jamii kuchukua jukumu la maendeleo yake. Tunataka kuunda mfano endelevu wa maendeleo ambao utaendelea kunufaisha jamii kwa muda mrefu baada ya mradi kukamilika,”amesema.

 Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Ngollo  Malenya, amesema kongamano hilo ni mwanga wa matumaini na fursa kwa wilaya hiyo, likilenga majadiliano, ushirikiano na kubadilishana mawazo ya kibunifu yanayoweza kuipeleka wilaya katika maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Vita Kawawa amesisitiza umuhimu wa wakazi wilaya hiyo kutumia kongamano hilo ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya kilimo na madini kwa kuwa ina uwezo mkubwa wa kuchangia uchumi wa nchi.

Aidha Kawawa ameomba msaada kutoka kwa mamlaka za serikali kusaidia mradi wa uchimbaji madini ya uranium wa Mantra wilayani humo, akiamini kwa  juhudi za serikali, mradi huo unaweza kuendelea angalau miaka 15 na kuchangia 20% ya pato la uranium barani Afrika na 4% ya uzalishaji  duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles