29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii yaaswa kuabudu bila ubaguzi

Seif Takaza, Iramba

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Askofu Yona Essya, ameitaka jamii kushirikiana katika shughuli za kijamii bila ubaguzi wa dini ili kudumisha amani nchini.

Askofu huyo wa Kanisa la TAG la Mjini Kiomboi, amesema hayo katika uzinduzi wa Kanisa la MMPT Mapampa Old Kiomboi yaani Muungano wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania, amesema kuwa bila amani hakuna mtu atakayefanya ibada, hivyo inapasa kila dhehebu lifanye ibada bila kubughudhiwa na jingine  kwa  lengo ni kwenda kwa Mungu.

‘Ndugu zangu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila mtu ana haki ya kuabudu dini anayotaka isipokuwa asivunje sheria, kama mnafanya ibada kwa amani hakuna atakayekuingilia hata Serikali haiwezi kutuingilia ili mradi tunafuata maadili ya dini na sheria za nchi.

“Wajibu wetu sisi viongozi wa dini ni kuhubiri dini kwa amani na njia sahihi ya kutupeleka mbinguni ,halikadhalika kuheshimiana waumini kuheshimu viongozi wao na sio kutengeneza makundi ya kupingana kwa kufanya hivo ni kumsaliti Mungu,” amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha Askofu Yona amewahimiza waumini wa kanisa hilo kuwa na umoja upendo na amani wanapokuwa kwenye ibada na kuwaomba wamche Mungu bila kubaguana wenyewe kwa wenyewe kwani kwa kufanya hivyo ni  usaliti.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la MMPT Mapampa, Lazaro Kitundu amewashukuru viongozi wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wa Serikali akiwemo Diwani wa Kata ya Old Kiomboi kuhudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa kanisa hilo.

‘’Natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya waumini wenzangu kwani Mwenyeti wa Kamati ya Amani Askofu Yona Seleman pamoja na Kamati yake ambayo iliyoko chini ya Mkuu wa Wilaya, Suleiman Mwenda wamesaidia sana kanisa hili kwa hali zote mpaka tumefikia hatua ya kuanzisha kanisa hili nawaombea Mungu awatie nguvu ili waweze kuongoza kwa haki upendo, busara na amani’amesema Mchungaji Lazaro

Katika uzinduzi huo, Askofu Yona alifanya Changizo la ujenzi wa kanisa hilo ambapo zilipatikana takribani shilingi milioni mbili ambapo lengo ni kujenga kanisa la kisasa ili liweze kukidhi kufanya ibada pamoja na ofisi ya kanisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles