27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

MAMA AMCHOMA MTOTO WAKE KWA KUIBA SH 7,000

ALLY BADI

-LINDI

MTOTO Razaki Ally (9), mkazi wa Kitongoji cha Milamba Kata ya Kivinje wilayani Kilwa, amelazwa  katika Hospitali ya Kinyonga, akiuguza majeraha  a baada ya kuchomwa moto mikononi na mama yake mzazi, Zabibu Issa  kwa tuhuma za kuiba Sh 7,000.

Razaki   ameunguzwa vibaya mikono yake yote miwili na kwa sasa hana uwezo wa kushika kitu chochote kutokana na majeraha hayo ya moto.

Akizungumza na MTANZANIA jana baada ya kutembelea hospitalini hapo, mama wa  mtoto huyo, Zabibu Binamu  alisema alichukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na tabia ya wizi na mashtaka ya kila wakati kutoka kwa majirani zake.

Alisema siku ya tukio, mtoto wake alimuibia   Sh 7,000 alizokuwa amezitunza chumbani kwake hali iliyomfanya achukie na kupatwa na hasira iliyosababisha kuchukua uamuzi wa kumchoma moto mikono yake.

 “Jamani  naomba nieleze ukweli kisa kwa ujumla mtoto wangu huyo amekuwa  na  tabia  ya wizi  na  udokozi mara  nyingi tu, hivyo hasira ilinipanda nikaamua kumchoma moto   kukomesha  tabia  hiyo,” alisema Zabibu.

Hata hivyo, mwanamke huyo mwenye watoto watatu, alisema anajutia kitendo alichokifanya, akidai kinampotezea muda wa kuendelea na shughuli zake za kujitafutia riziki ikizingatiwa hana mume.

Mmoja wa mashuhuda,  Mwanaharusi Kumala, ailiambia MTANZANIA  kuwa siku hiyo ya tukio, Razaki akiwa nyumbani kwao alimsikia mtoto huyo akipiga kelele za kuomba msaada baada ya kuchomwa moto na mama yake.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kinyonga, Dk. Salehe Abubakari, alikiri kumpokea mtoto  huyo akiwa na majeraha kutokana na kuchomwa moto na mama yake mzazi kwa madai ya kumuibia fedha.

Alisema kutokana na kiwango kikubwa alichoungua  mtoto huyo,  uchunguzi unaonyesha hali hiyo inaweza  kumsababisha kupata ulemavu wa kudumu.  

Mwenyekiti  wa  Jukwaa la  Wanawake  wilaya  Kilwa, Tumainieli Mpunga, ameiomba Serikali kuwachukulia hatua za sheria  wazazi, walezi na watu wengine  walio na tabia ya ukatili dhidi ya watoto, kama alivyofanya Zabibu.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga   alikiri kulifahamu suala hilo lakini hakuwa tayari kulieleza kwa kina kutokana na kuwa nje ya ofisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles