21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Makonda apokea msaada wa ndoo 500 za rangi

Brighiter Masaki-Dar es salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepokea msaada wa ndoo 500 za rangi kutoka kampuni ya rangi ya Billion Point kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa 381 kwa wanafunzi 5,970 walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makonda aliwashukuru wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa kuamua kuunga mkono juhudi za Serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini.

Mchango huu ni muhimu kwa sababu Rais wetu (Dk. John Magufuli) anatoa elimu bure na kwenye mkoa wetu takribani watoto 5,970 katika wilaya moja tu ya Temeke, walikosa madarasa na sasa tupo kwenye ujenzi wa madarasa 381, hivyo tuwashukuru wazawa kwa kuitikia mwito hasa kwenye sekta ya elimu.

“Ndoo 500 zitakuwa ni mchango mkubwa sana ambao hauwezi kusahaulika, tutapaka rangi na kuandika jina lako kwenye darasa moja kama ishara ya shukurani,” alisema Makonda.

Aliwataka vijana kuacha kukaa mitaani na kulalamika kuwa ajira ni ngumu, badala yake wajitume kutengeneza viwanda na kutoa ajira kwa vijana wengine.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni ya Billion Point, Lucy Muluve, alisema wamejitoa kwa sababu ni nyumbani na kwa kuwa wanafunzi wanatakiwa kupata elimu kwenye mazingira mazuri na yenye ushawishi wa kusoma kwa bidii.

Kwa upande wake, Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, aliwaagiza wakuu wa mikoa wote nchini kuhakikisha hadi kufikia Februari 28, wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili ifikapo Machi Mosi wanafunzi waliokosa masomo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, waanze masomo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,719FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles