29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Makamba aanika mafanikio, mwelekeo mpya Tanesco

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema mabadiliko yanayofanywa katika Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) yameleta mafanikio makubwa kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwake.

Kwa mwaka 2021/22 shirika hilo limerekodi mapato ya Sh trilioni 2.3, faida ya Sh bilioni 109.4 huku thamani ya mali ikifikia Sh trilioni 19.

Baadhi ya viongozi wa serikali, wakuu wa taasisi na wabunge wakifuatilia uzinduzi wa taarifa ya mwaka na npango kazi wa Tanesco, Dar es Salaam.

Akizungumza Jumatatu Julai 31,2023 wakati wa uzinduzi wa taarifa ya mwaka 2021/22 na mpango mkakati wa miaka 10 ijayo, amesema dhamana ya shirika hilo kwa maendeleo ya nchi ni kubwa hivyo lazima lifanye mambo makubwa.

“Shilingi bilioni 109 ni faida ya kihistoria, tumepata mafanikio lakini safari bado ni ndefu sana, lakini dalili ni nzuri.

“Tunaomba subira, mtupe muda kwa sababu mabadiliko yanachukua muda mrefu…mabadiliko yanayofanyika Tanesco yanaweza yasieleweke mwanzoni, itabidi tuzoee namna ambavyo mambo yanafanyika,” amesema Makamba.

Hata hivyo amesema faida iliyopatikana haitoshelezi hivyo bado wataendelea kutegemea mtaji wa Serikali na sekta binafsi katika uwekezaji wa umeme.

Naye Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema kutokana na mabadiliko iliyoyafanya Tanesco kuanzia Septemba mwaka huu itarudishiwa mamlaka yake ya kuweza kuajiri na kushughulikia masuala ya masilahi.

Hata hivyo ametahadharisha uhuru huo uwe wa uwazi na uwajibikaji kwa kuzingatia vigezo walivyokubaliana.

“Mabadiliko ya utendaji katika taasisi zetu ni jambo lisiloepukika, tusipofanya marekebisho kila siku tutakuwa watu wa kunyosheana vidole na lazima tubadilike katika hilo.

“Kila taasisi lazina wajitahidi kuwa wazi, kuwasilisha ripoti za mwaka na kuwa na mikakati na kuiwasilisha,” amesema Mchechu.

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lindam Group, Zuhura Muro, ameshauri Tanesco iendelee kuhakikisha nishati inapatikana kwa gharama nafuu na kuwafikia wananchi wengi hasa wanawake ili waweze kuzalisha na kuchangia pato la taifa zaidi.

Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande, amesema kutokana na mikakati waliyonayo wanaamini kufikia mwaka 2026/27 matatizo mengi yatakuwa yamekwisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles