25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makala| NMB inavyotumia faida yake kusukuma maendeleo kwa jamii

Na Derick Milton, Mtanzania Digital

Ushiriki wa taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali katika shughuli za maendeleo kwa jamii husika ni jambo la muhimu kwenye maendeleo yoyote ya nchi hasa katika mataifa yanayoendelea.

Suala la maendeleo kwa jamii, halijaachwa tu kwa Serikali kuwa ndiye mwenye wajibu pekee katika kulitekeleza kama ilivyo dhana kwa wengi, bali halina budi kutekelezwa na kila mdau wa maendeleo iwe sekta ya umma ua binafsi.

Meneja Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospter Magesse akimkabidhi Madawati Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Festo Kiswaga kwa ajili ya Shule ya Msingi Majengo.

Serikali kama mdau mkuu wa Maendeleo nchini, imeendelea kutekeleza wajibu wake kila mwaka kwa kupeleka huduma mbalimbali za jamii karibu na wananchi ikiwemo Elimu, Afya, Maji na nyingine nyingi.

Katika sekta ya elimu na afya, serikali imeweza kujenga shule nyingi za msingi na sekondari. Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ikiwemo kuboresha mazingira ya utolewaji wa huduma hizo kila wakati.

Hata hivyo, licha ya wananchi kusogezewa huduma hizo karibu na makazi yao, bado sekta hizo zimeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali za ukosefu wa raslimali watu, fedha na vifaa vya kutolea huduma.

Uwepo wa changamoto hizo kwa namna moja au nyingine bado haujaathiri kwa kiwango kikubwa dhana ya serikali ya kusogeza huduma kwa jamii, bali zimeendelea kutolewa lakini siyo kwa kiwango ambacho kimekusudiwa.

Kwa upande wa sekta ya elimu, serikali imeendelea kujenga shule nyingi za Msingi na sekondari kwa kushirikiana na wananchi lengo likiwa kupunguza adha kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Hatua ya ujenzi wa shule nyingi imepelekea kuwepo changamoto ya upungufu wa walimu, upungufu wa miundombinu mbalimbali yakiwemo madarasa, vyoo, ofisi za walimu pamoja na madawati au meza.

Upande wa afya pia hivyo hivyo ujenzi wa zahanati kila kijiji, vituo vya afya kila kata, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa za mikoa ndiyo sera ya serikali ambayo imeendelea kuitekeleza kwa kasi.

Vituo hivyo vya kutolea huduma za Afya vimeendelea kujengwa kwa kiwango kikubwa hasa maeneo ya Vijiji, ambapo ongezeko lake limeendelea kuzua changamoto mpya ikiwemo upungufu wa vifaa tiba mbalimbali, pamoja na watumishi.

Lengo la serikal kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi limetimia, lakini bado limeendelea kuzalisha changamoto mpya ambazo wadau wa mbalimbali wa maendeleo utakiwa kushiriki katika kuhakikisha huduma bora kwa jamii zinapatikana.

Kupitia mnyororo huo wa ushiriki shughuli za Maendeleo, Benki ya NMB Tanzania, ilianzisha sera yake inayoitwa “Kurudisha kwa Jamii”.

Kupitia sera hiyo NMB ilichagua sekta mbili ambazo ni Afya na Elimu, ambapo kupitia faida ambayo imekuwa ikipata kila mwaka basi asilimia moja ya faida urejeshwa kwa jamii kusaidia shughuli za Maendeleo kwenye sekta hizo.

Kutokana na sekta hizo kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na kwa kiwango kikubwa, NMB kupitia sera yake imeendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa kuboresha utolewaji wa huduma kupitia sekta hizo.

Kwenye elimu NMB imeendelea kushiriki mazingira ya utolewaji wa huduma bora katika sekta hiyo kwa kutoa madawati, meza, ujenzi wa madarasa, kwenye shule za msingi na sekondari.

AFYA

Afya nako NMB imeendelea kushiriki kuboresha huduma za Afya kwa kusaidia kutoa vifaa tiba mbalimbali kama vitanda vya wagonjwa, vitanda vya wajawazito kujifungulia, mashuka, magodoro lakini pia ujenzi wa zahanati, vituo ya Afya na hospitali za Wilaya na Mikoa.

Mikoa ya Simiyu, Kigoma, Tabora, Shinyanga na Geita ni kati ya Mikoa ambayo imeendeela kunufaika na uwepo wa NMB kupitia sera yake ya kurejesha kwa jamii.

Kupitia kanda yake ya Magharibi ambayo inaundwa na mikoa hiyo, NMB imeendelea kutoa vifaa mbalimbali katika sekta ya Afya na Elimu kwa kutoa madawati, meza, vifaa vya ujenzi vyumba vya madarasa pamoja na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa ndani ya hiki hii vimegharimu kiasi cha Sh milioni 65,540,000 na vimetolewa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari, vituo vya kutolea huduma za afya katika mikoa ya, Shinyanga, Kigoma, Tabora na Geita.

Katika mkoa wa Kigoma NMB ilikabidhi vitanda 10, magodoro na shuka 50 vyenye thamani ya Sh milioni sita kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Uvinza kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

ELIMU

Aidha, katika Wilaya ya Kasulu mkoani humo NMB ilitoa viti 50 pamoja na meza zake katika shule ya sekondari Nkundutsi vyenye thamani ya Sh milioni tano ikiwa ni kuunga mkono serikali katika uboreshaji wa miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia kwa shule za Msingi na Sekondari.

Katika mkoa wa Geita Benki hiyo ilitoa madawati 100 yenye thamani ya Sh milioni 15 kwa ajili ya shule ya msingi Muyama, huku katika Wilaya ya Bukombe ikitoa mabati 116 yenye thamani ya Sh milioni 3.7 na Mbogwe madawati 50 yenye thamani ya Sh milioni 4.5.

Mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kahama Benki hiyo katika kuendeleza sera yake ilikabidhi madawati 250, na viti na meza 50 vyenye thamani ya Sh milioni 24.5 kwa shule nne za msingi na sekondari moja kwenye halmashauri ya Ushetu na Manispaa ya Kahama.

Shule za Msingi Ubagwe madawati 50, Ushetu 50, Mapamba 50 , zote za halmashauri ya Ushetu na kwa upande wa Manispaa ya Kahama ni shule ya Msingi Majengo madawati 50, Ubagwe Madawati 50 na sekondari ya Kisuke ikisaidiwa Meza na viti 50, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 24.

Katika Mkoa wa Tabora wilayani Uyui NMB ilikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh milioni 10 ambavyo ni mabati 300 na mbao 180 kwa ajili ya shule ya Msingi Loya na Mwisole.

BAJETI INAYOTENGWA NA NMB

Sospeter Magesse ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa nyakati mbalimbali anasema kuwa anasema kuwa NMB inatoa vifaa hivyo lengo likiwa kuendeleza sera ya benki hiyo katika kusaidia huduma za jamii na hasa sekta za kipaumbele za elimu na afya.

Anasema kuwa Benki ya NMB imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mipango ya benki kila mwaka kusaidia huduma mbalimbali za kijamii hasa huduma za afya na elimu na kwamba mpango huo unalenga kurudisha kwa wananchi faida ambayo benki hiyo inaingia wananchi wakiwa sehemu ya mchakato huo.

Anaibainisha kuwa kila mwaka NMB imekuwa ikitenga kiasi cha Sh bilioni moja kwenye faida wanayoipata kusaidia sekta ya elimu na afya ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.

“NMB inatambua ndani ya jamii kuna mahitaji mengi ya msaada lakini kipaumbele chetu kipo kusaidia kwenye sekta ya elimu na afya ambazo nimtambuka kwa jamii, tunatambua madawati kwa watoto ni sehemu ya kuwafanya wasome katika mazingira mazuri na kufanya vizuri katika suala la kitaaluma,” anasema Maggese.

Anabainisha kuwa kwa upande wa kutoa huduma benki ya NMB itaendelea kuwasogezea huduma jamii katika maeneo yao kwa kuongeza matawi na mawakala katika maeneo yao na kuwataka watu kujitokeza kuitumia fursa mbalimbali zinazotolewa za kiuchumi ikiwemo mikopo ya kilimo na biashara.

Katika kutambua mchango wa Benki hiyo, serikali imeendelea kuipongeza NMB kwa kujali jamii huku, huku wadau wengine wa maendeleo zikiweo sekta binafsi kuiga mfano wa Bneki hiyo katika kujali jamii.

Festo Kiswaga ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakati akipokea vifaa kutoka Benki hiyo, aliishukuru benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya elimu kwa msaada huo utakao wasaidia watoto waweze kusoma kwenye mazingira mazuri ya kukaa katika madawati.

Kiswaga alisema dhamila ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watoto wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati na kwa mdaasa huo katika shule za msingi nne na sekondari moja utakuwa umepunguza changamoto hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Isack Mwakisu alisema kuwa kuboreshwa kwa miundo mbinu ya shule na kuwepo kwa madawati kuna mchango mkubwa katika kuongeza ufaulu kwa wananfunzi.

Mwakisu alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika hilo lakini haiwezi kutimiza kila kitu kwa wakati mmoja hivyo kuwepo kwa msaada kama huo kutoka kwa wadau wa maendeleo kuna maana kubwa katika mpango wa wadau huo kuunga mkono serikali kwenye mchakato wa maendeleo.

Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Ushetu, Velena Ntulo kwa niaba ya mkurugenzi alisema wanakabiriwa na upungufu wa jumla ya madawati 8300 na kwa msaaada huo wanaishukuru benki ya NMB kwa kuwasaidia kupunguza changamoto hiyo.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Ofisa michezo Lupola Nkomwa alIshukuru kwa msaada huo kwa kuona umuhimu wa mtoto kusoma vizuri akiwa amekaa kwenye dawati hali inayowasaidia kuwa na mwandiko mzuri na utoro mashuleni unaotokana na kukaa chini.

Meneja Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospter Magesse akimkabidhi Mabati Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Kisari Makori kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Loya pamoja na Mwisole vifaa ambavyo vimetolewa na Benki hii ili kuunga mkono juhudi za wananchi katika kukamilisha ujenzi wa Madarasa.

Kwa upande wao baadhi ya walimu wa shule zilizopokea msaada huo wamesema kuwa msaada huo utakuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri na yenye kuvutia kwa kuwa wanafunzi wamekuwa wakikaa wengi kwenye dawati moja hali ambayo ilikuwa ni chagamoto katika kuandika.

Vickness Desdery ni Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Muyama wilaya ya Buhigwe akizungumzia msaada huo alisema kuwa utasaidia kuboresha taaluma kwani kukaa chini au kwenye mawe au kubanana kwenye dawati kuwaathiri kiasi kikubwa katika muandiko lakini pia kuwa makini katika masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles