26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

MAHREZ: NIMECHAGUA ALGERIA KUMUENZI BABA

 Riyad Mahrez
Riyad Mahrez

LIBREVILLE, GABON

NYOTA wa timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez, ameweka wazi kuwa alifanya maamuzi ya kuchagua kuitumikia timu hiyo badala ya Ufaransa, kumuenzi marehemu baba yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amedai kuwa alikuwa na nafasi ya kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa ambapo amekulia huko, lakini aliamua kufanya maamuzi ya kuitumikia Algeria ambako baba yake alizaliwa.

Hata hivyo, maamuzi hao aliyafanya mara baada ya baba yake kupoteza maisha mwaka 2006, hivyo Mahrez alifanya maamuzi hayo mwaka 2014.

Mchezaji huyo alitwaa uchezaji bora wa Ligi Kuu nchini England msimu uliopita baada ya kuisaidia klabu yake ya Leicester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo, pia alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ambaye anacheza soka Ulaya, tuzo ambazo zilitolewa na Shirika la Utangazaji la BBC.

“Ni jambo la furaha kulitumikia taifa la Algeria ambako baba yangu alitokea, nilizaliwa nchini Ufaransa na nilikuwa na kila sababu ya kufanya maamuzi ya kucheza soka ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa lakini sikuona sababu.

“Nimeamua kufanya maamuzi ya kucheza nchini Algeria kumuenzi baba yangu ambaye alipoteza maisha tangu mwaka 2006, hakuwahi kuyaona mafanikio yangu, acha nifanye hivi kwa ajili yake, ninaamini ubora wa kikosi hiki utatufanya tufanikiwe kutwaa taji la Mataifa ya Afrika msimu huu,” alisema Mahrez

Timu hiyo leo inatarajia kushuka dimbani kwa mchezo wake wa kwanza katika ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Zimbabwe, huku mchezo wa pili ni kati ya Burkina Faso dhidi ya Cameroon, michezo yote itapigwa kwenye uwanja wa Stade d’ Angondje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles