23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI YATANGAZWA RASMI

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Na Mwandishi wetu,

Jumla ya wanafunzi 36,737 ambao ni sawa na asilimia 8.98 watarudia kidato cha pili mwaka huu kwani wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Aidha, wanafunzi 67,547 sawa na asilimia 6.64 waliopata alama E kwenye upimaji wa Kitaifa wa darasa la nne (SFNA) nao watarudia darasa hilo.

Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde leo alipokuwa akitangaza matokeo ya mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA), 2016 pia ule wa darasa la nne (SFNA).

Alisema takwimu za matokeo ya upimaji wa FTNA zinaonesha jumla ya wanafunzi 372,228 pekee sawa na asilimia 91.02 wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Aliongeza kuwa kati ya hao waliofaulu wasichana ni 189,161 sawa na asilimia 90.27 na wavulana 183,067 sawa na asilimia 91.80.

Alisema matokeo hayo yanaonesha ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya msingi Uraia, Historia, Jiografia, Fizikia, Biolojia, Kiswahili na Hisabati umepanda mwaka 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles