25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Nitashusha bei ya saruji, mabati

Pg 1 magufuliNA BAKARI KIMWANGA, TUNDURU

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema endapo atachaguliwa kuongoza Serikali ya awamu ya tano, atahakikisha anashusha bei ya saruji na mabati ili kila Mtanzania aweze kufurahia
maisha kwa kujenga nyumba bora na nzuri.

Amesema hatakuwa tayari kuona bei ya vifaa vya ujenzi ikipaa hali ya kuwa viwanda vipya vitaanza uzalishaji.

Kauli hiyo aliitoa jana katika mikutano yake ya kampeni za kuomba kuchaguliwa kuwa rais katika wilaya za Namtumbo, Tunduru mkoani Ruvuma na Masasi mkoani Mtwara, ambapo alisema amejipanga kuwatumikia Watanzania kwa dhati kwa kuleta mageuzi ya kiuchumi.

“Kuanzia mwaka kesho tutashusha bei ya saruji na mabati ili kumwezesha kila Mtanzania popote alipo aweze kujenga nyumba bora. “Hivi sasa tunajenga kiwanda kikubwa cha kisasa pale Mtwara (Dangote) cha saruji ambacho
ni kikubwa katika nchi za Afrika Mashariki.

“Na sasa muda mfupi ujao kitaanza uzalishaji na sisi Mkoa wa Ruvuma tujiandae kwa kupokea mapinduzi ya maendeleo na kiuchumi bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini na hata ukabila,”

alisema Dk. Magufuli. Akizungumzia kuhusu uhusiano, alisema Serikali yake itaendelea kuimarisha uhusiano na nchi zote jirani kama ilivyokuwa katika awamu zilizopita.

Dk. Magufuli alisema katika kuhakikisha nchi inaendelea, itakuwa karibu na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
Alisema anaomba achaguliwe yeye ndio mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania pamoja na nchi za Ulaya.

“Nichagueni mimi naaminika na nchi zote, msichague mtu asiyeaminika mbele ya wahisani, kama mtachagua mtu wa aina hiyo wahisani wanaweza wasiendelee kutoa misaada.

“Nilikuja hapa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara na Rais Kikwete, na sasa kazi inaendelea na
ujenzi.

“Lengo la Serikali ya CCM ni kuiunganisha nchi kwa mtandao wa barabara, na sasa Jaica wapo wametupatia fedha kwa ajili ya ujenzi Namtumbo hadi Mtambaswala mkoani Mtwara,” alisema.

Akizungumzia madini ya uranium yalipo wilayani Namtumbo, alisema Serikali yake itayaendeleza ili yaweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi.

AKAGUA BARABARA

Akiwa njia kuelekea Tunduru, Dk. Magufuli, alijivua kwa muda kofia ya ugombea na kulazimika kurejea katika nafasi yake ya Waziri wa Ujenzi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara katika Kijiji cha Uliya.

Akiwa hapo alisema kazi ya ujenzi wa barabara ni lazima ikamilike kwa wakati.
“Endeleni na kazi ya ujenzi na huyu mkandarasi tumeshamlipa fedha zote na hadai.

Niwaombe nyie vibarua msigome na Serikali itasimamia masilahi yenu bora kwa wakati.
“Awali alikuwepo mkandarasi Progressive, amefanya mambo ya ajabu tumemfukuza na sasa kazi inaendelea,” alisema Dk. Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles