30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

MAGUFULI AMTEUA BLANDINA NYONI

RAIS Dk. John Magufuli

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Blandina Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema kuwa Nyoni ambaye uteuzi wake umeanza jana, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Zakhia Meghji aliyemaliza muda wake.

Mwaka 2012, Nyoni alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya Awamu ya Nne, lakini aliondolewa katika nafasi hiyo baada ya kuwapo kwa mgomo wa madaktari.

Mbali na Nyoni, pia Rais Magufuli amemteua Dk. Baghayo Saqware kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Taarifa hiyo ilisema kuwa uteuzi wa Saqware aliyechukua nafasi ya Israel Kamuzora aliyestaafu unaanza mara moja.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk. Saqware alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles