Madaktari wapiga kambi kutoa vipimo magonjwa yasiyoambukiza

0
890

Florence Sanawa, Mtwara

Timu ya Madaktari wa kituo cha Ilala Afya Centre imepiga kambi ya Siku mbili Katika kituo cha afya Likombe  Manispaa ya Mtwara Mikindani kutoa vipimo vya magonjwa yasiyoambukiza.

Magonjwa hayo ambayo ni kisukari, Saratani ya Shingo ya mlango wa kizazi, macho, meno na Matiti ambapo upimaji huo umedhaminiwa na taasisi 15 ikiwemo machinga high class Huku timu ya madaktari wa kawaida watano (5) na madaktari bingwa wanne (4) wakiongeza nguvu ya upimaji wa magonjwa hayo ambapo wanatarajia kuona wagonjwa 2500 ndani ya siku mbili.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Zainab Sachak mratibu wa vituo vya kutolea huduma  za afya hospitali ya ilala afya centre alisema kuwa kutokana na wingi wa wagonjwa watalazimika kutoa huduma hadi usiku.

“Huwa tunashirikiana kwa ukaribu na ocean road hii ni kambi ya nne, tanga tuliona watu 1600 na mtwara hadi sasa ni saa sita lakini watu 1100 tayari wameshachukua namba tutaangali ili tuweke utaratibu wa kutoa huduma hii mara kwa mara ila hawa waliochukua namba tutawapa wote huduma hata iwe usiku na tutawamaliza wote walikuwa na namba”

Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni ya Machinga Transport Services Hasnain Murji alisema kuwa kampuni hiyo iliona uwepo wa uhitaji wa afya hiyo hali iliyowalazimu kufanya mawasiliano na ilala health centre kwaajli ya kuja kupiga kambi katika eneo hilo.

“Sio tu vipimo pia madaktari waliokuja hapa wamekubali endapo mtu atakutwa na tatizo lolote atapelekwa kwa matibabu zaidi ambapo hata usafiri watatumia wa kampuni yetu lakini tunaona juhudi kubwa zilizofanywa na Mganga mkuu wa manispaa ya mtwara mikindani ni mara chache sana kuona mtumishi wa serikali akijitoa kama alivyojitoa” alisema Murji

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here