23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mabondia Emmanuel Shija na Yusuph Fundi kupanda ulingoni Jumamosi hii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bondia raia wa Tanzania, Emmanuel Shija pamoja na Yusuph Fundi tayari wamekamilisha zoezi la kupima uzito kwa ajili ya pambano lao kwenye ulingo wa Bongo Fighting Championship litakalofanyika Jumamosi hii Julai 29, 2023.

Zoezi hilo la kupima uzito limefanyika mapema leo Julai 28,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam ambapo mabondia mbalimbali wamejitokeza kwa ajili ya uthibitisho wa awali kabla ya kupanda ulingoni.

Muasisi wa pambano hilo, Scott Farrel amepima uzito kuelekea pambano la kirafiki dhidi ya mpinzani wake Marcus Warry, Abdul ubaya dhidi ya Ivan Maguma wakati Musa Dragon dhidi ya Amos kutoka Kenya wakati Ajemi amani dhidi Khamis msondo, Huku pambano la Muhaythai huku pambano kuu ni Emmanuel Shija dhidi ya Yusuph Fundi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa amesema wamejipanga kurusha maudhui yote yatakayojiri katika pambano hilo.

“Bongo fighting championship ni pambano lenye lengo la dhati na wazi kutoa ushirikiano kwa mabondia kutumia platform ya Startimes ndani ya Tv3 kuonekana mwanzo mwisho kwa maudhui yote na kipekee watashuhudia la pambano Mwanamke Feriche Mashauri dhidi ya Chiedza Homakoma kutoka Zimbabwe,” amesema Malisa.

Kwa upande wake, Feriche Mashauri amesema ameshukuru kwa kufika salama mpinzani wake Homakoma kutokana na tatizo kubwa linaloukumba mchezo wa masumbwi kutofika kwa wapinzani nchi husika ya pambano kwa kusingizia changamoto ya usafiri.

Hata hivyo, amesema amejiandaa vizuri kumkabili mpinzani wake huku akificha kumpiga Ko raundi ya ngapi akiwaacha mashabiki kushuhudia mchezo huo kupitia tv3 au kufika ukumbi wa Superdome Masaki jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles