21.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

LUPITA AWAPA NENO WAREMBO AFRIKA

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa filamu nchini Marekani mwenye asili ya nchini Kenya, Lupita Nyong’o, amewataka warembo barani Afrika kujivunia urembo wa rangi zao ili kulitangaza bara lao.

Mshindi huyo wa tuzo za Oscar, amedai kwa upande wake anajivunia rangi pamoja na mwonekano wa nywele zake za Kiafrika katika kazi zake za mitindo na burudani.

“Nimekuwa nikipata kazi mbalimbali kutokana na rangi yangu na nywele za Kiafrika, nafanya vizuri katika tasnia ya filamu Hollywood kama walivyo watu wengine.

“Hivyo huu ni wakati wa wasichana wengine wenye rangi na nywele kama zangu kujivunia vile walivyo, hakuna sababu ya kujibadilisha kwa ajili ya kutaka kufanana na watu fulani, kila mmoja ajivunie kile alichopewa na Mungu,” alisema Lupita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles