30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

LUKUVI ‘AMNYANG’ANYA’ MAKONDA KIWANJA ALICHOPEWA NA MFANYABIASHARA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara Mohamed Ikbar kwa kumgawia kiwanja cha serikali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimdanganya ni mali yake.

Waziri Lukuvi amesema hayo leo wakati akitangaza wizara yake kuhamia rasmi Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine amekirudisha kiwanja hicho kwa serikali kwani  kiwanja hicho ni mali ya wananchi tangu aliposhindwa kesi aliyoifungua mwenyewe mahakamani.

“Yule ambaye amemdanganya Makonda kwamba amempa ardhi kigamboni, ile ardhi hakumpa amemdanganya na sisi tutamsaidia Makonda kuchukua hatua kwa sababu ile ardhi ni ya wananchi na serikali ilikuwa inafanya mazungumzo na wananchi akawashtaki mahakamani akashindwa leo anakwenda kujipendekeza kwa Makonda.

“Ile ardhi si yake kwa sababu wananchi walishashinda, siwezi kumdanganya Mkuu wa Mkoa kuwa umeidanganya serikali kwa sababu Makonda hakuomba yeye ndiyo amepewa, kwa sababu amemdanganya na mimi ndiyo custodian (msimamizi) wa ardhi nitamsaidia Makonda kuchukua hatua ili angalau watu wasijipendekeze namna hii kusafisha maovu yao kwa kutumia mgongo wa viongozi,” amesema Lukuvi.

Aidha, amesema wazo la Makonda kwamba eneo hilo liwe la viwanda ndilo wazo la serikali kuwa libaki kuwa eneo la viwanda na dampo. Lakini pia amewataka watu wote wanaomiliki ardhi kukiorodhesha katika vitabu vya wizara wilayani ili wapatiwe hati kuanzia sasa hadi Juni 30, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles