23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Lissu, Bulaya waingia Kamati Kuu Chadema

lisu-na-bulaya

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefanya uchaguzi wa wajumbe watano wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwakilisha kundi la wabunge.

Taarifa iliyotolewa jana   na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, ilieleza kuwa katika uchaguzi huo ulifanyika   Dodoma jana,   uliwachagua Tundu  Lissu, Godblesss Lema, Joseph Mbilinyi, Ester Bulaya na Mariam Salum Msabaha kuwa wajumbe wa Kamati Kuu.

Alisema  kutokana na Serikali kuamua kupuuza maoni Kamati Kuu ya Chadema katika kikao chake cha kawaida kilichoketi Oktoba 22-23, jijini Dar es Salaam,  iliazimia kutuma ujumbe wa baadhi ya wajumbe waandamizi wa Kamati Kuu kwenda Dodoma kukutana na wabunge wa Chadema kujadiliana na kutoa maelekezo ya chama.

Wajumbe walioteuliwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profesa Abdallah Safari, Profesa Mwesiga Baregu, Arcado Ntagazwa na Mawaziri wakuu wa zamani ambao pia ni wajumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles