30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Lissu akamatwa mkoani Singida

Tundu LissuNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake.

Akithibitisha kukamatwa kwake jana jioni, alisema kuwa  baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Ikungi, alifutwa na Ofisa wa Polisi na kumwalifu kuwa anahitajika polisi kwa mahojiano.

“Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki.

“ Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe. Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

“Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely nitasafirishwa Dar usiku huu (jana). In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa,sitakubali kunyamazishwa Aluta continua,” alisema Tundu Lissu katika ujumbe wake uliombazwa jana jioni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles