22.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

Lil Ommy akimbiza tuzo za AEA USA

Na CHRISTOPHER MSEKENA

MTANGAZAJI nyota wa vipindi vya burudani Bongo, Omary Tambwe ‘Lil Ommy’, amewashukuru mashabiki kwa kuendelea kumpigia kura kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA za Marekani.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lil Ommy ambaye kwa mara ya pili anawania kipengele cha Mtangazaji Bora wa Mwaka Afrika (Best Host), alisema sasa mashabiki wanaweza kuendelea kupiga kura baada ya juzi mfumo wa kura kuzidiwa na wingi wa watu waliokuwa wanampigia kura.

“Tuendelee kupiga kura za kutosha kwenye kipengele cha Mtangazaji Bora wa Mwaka Afrika (AEA USA) ije tena Bongo kwa Bonyeza link kwenye bio yangu Instagram kisha nenda mpaka kipengele namba 24 chakua jina la Lil Ommy, ingiza jina lako na nchi ulipo kisha piga kura (vote), huu ndio mfumo mpya baada ya ule wa awali kugoma na sasa umerudi tena, tuendelee kupiga kura,” alisema mtangazaji huyo wa The Switch ya Wasafi Fm ambaye ameingia kwenye orodha ya mastaa wachache wenye wafuasi zaidi ya milioni 1 kwenye Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles