31.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

LIBYA YATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO

 

TRIPOLI, Libya


Ujumbe  wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini hapa, umesema kwamba, makundi yanayopigana na Serikali yamesaini mkataba wa kusitisha mapigano makali kati ya makundi hayo na wanajeshi wa Serikali.

Tangazo hilo limekuja baada ya siku nane za mapigano makali baina ya wanamgambo wa wapiganaji wanaohusishwa na mamlaka ya kimataifa kutambuliwa katika mji mkuu huu na wengineo kutoka nje ya mji huu.

Hili ni mara ya tatu kufikiwa makubaliano kama hayo katika harakati za kujaribu kumaliza mapigano na vurugu na ukatili unaoendelea mjini hapa. Majaribio ya awali ya kumaliza mapigano yalikufa mara baada tu ya kufikiwa.

Wakati huu utiwaji saini wa makubaliano ya kumaliza mapigano kumeidhinishwa na umoja wa mataifa, miongoni mwa makubaliano ni kukomesha maadui wote, kuwalinda raia na ombi la kufunguliwa kwa uwanja mkuu wa ndege ulioko mjini hapa ambao ulifungwa siku nne zilizopita kutokana na ghasia na mapigano.

Hata hivyo, mpaka sasa haijawa wazi  juu ya taarifa za kina kuhusu kile kilichoridhiwa katika makubaliano hayo ya kusitisha mapigano ingawa vikundi vidogo vidogo vyenye silaha vilivyoshiriki katika siku nane za mapigano makali, kimetoa taarifa kuwa kamanda wa vikosi vyao anaunga mkono suluhu.

Kikundi hiki kinadai kwamba, makubaliano ni pamoja na kuondoka kwa wapinzani wake kutoka mjini hapa.

Wapinzani hao ni vikosi vya kijeshi ambavyo vinahusishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Tripoli.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles