24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lembeli awatadharisha wananchi Shinyanga

LEMBENa Kadama Malunde

MGOMBEA ubunge wa   Kahama mjini   kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), James Lembeli,  amewataka watanzania kupuuza propaganda inayoenezwa kuwa mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli,  ni msukuma ili kuwarubuni watu wa Kanda ya Ziwa wampigie kura.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao za Ukawa katika Wilaya ya Shinyanga uliofanyika jana katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga, Lembeli alisema siyo kweli kwamba Magufuli yuko pamoja na watu wa Kanda ya Ziwa.

Lembeli alisema hakubaliani na propaganda inayoenezwa na wafuasi wa CCM  kuwa kwa vile Magufuli ni msukuma hivyo wasukuma wamuunge mkono kwenye mbio zake za kuutaka urais.

“Sikubali kabisa, mimi nilikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza dhambi na shida waliyopatiwa wafugaji wakiwamo wasukuma ambao waliuawa, waliteswa na kuibiwa mali zao lakini Magufuli anayedaiwa kuwa ni msukuma hakufungua mdomo wake kutetea ndugu zake,hatukubali,” alisema Lembeli.

Lembeli alisema   a kitendo hicho cha kukaa kimya dhidi ya vitendo viovu walivyotendewa wafugaji hao, inadhihirisha kuwa hayuko pamoja na wasukuma hivyo asionewe huruma bali watanzania wamchague Edward Lowassa ambaye ni jasiri na msema kweli.

Mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Shinyanga mjini, Patrobas Katambi, aliwataka wakazi wa Shinyanga kushikamana na kuepuka vitendo vya usaliti na kuhakikisha kuwa wanawapa kura wagombea wa Ukawa badala ya kuishia  kushangilia katika mikutano ya hadhara.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles