24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kunenge amtaka mkandarasi wa Makongo kumaliza barabara mwezi Oktoba

Brighter Masaki -Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amemtaka mkandarasi kutoka kampuni ya JASCO Building and Civil Contractor anaejenga Barabara ya Makongo kuhakikisha inakamilika kabla ya Mwezi October.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati wa ziara ya kukagua miradi minne ya maendeleo Jijini humo Kunenge amezitaka Taasisi za Dawasa na Tanesco kufanya kazi kwa ushirikiano na Mkandarasi huyo ili kukamilika kwa wakati.

“Niwaombe Dawasa na Tanesco kushirikiana na Mkandarasi, kwa kuondoa miundombinu ya Maji na umeme iliyopita kwenye mradi ili mkandarasi asipate kisingizio chochote cha kuchelewesha kazi.”

Aidha Kunenge amesema Barabara hiyo yenye urefu wa Km 4.5 ni moja ya Barabara muhimu Katika kutatua changamoto ya foleni kwenye Barabara ya Bagamoyo ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Bilioni 8.2.

Pia Kunenge ametembelea Ujenzi wa Barabara ya Madale kuelekea Wazo yenye urefu wa Km 6 inayogharimu Shilingi bilioni 9.7 ambapo amemuelekeza Mkandarasi kutoka kampuni ya MECCO kukabidhi Mradi mwezi wa tano mwishoni.

Kutokana na Barabara hiyo kuwa msaada mkubwa kwa Mabasi yaendayo Mikoa ya kaskazini yakitokea kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

Akiwa kwenye Ujenzi wa Daraja la Ulongoni A na B unaokwenda sambamba na ujenzi wa Barabara na kingo za mto, RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa Maagizo aliyowapa wakandarasi Jambo likilosaidia Ujenzi kufikia 70%.

Kutokana na hilo Kunenge ametaka Daraja la Ulongoni A kukamilika kabla ya Tar 10/06/2021 huku Daraja la Ulongoni B akitaka likamilike kabla ya Mwishoni mwa mwezi wa Sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles