24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Serikali itaendelea kutatua changamoto za vijana

Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim amezindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na maendeleo kwa Vijana balehe kwa Mwaka 2021/2022 hadi 24/25 huku akisema Serikali itaendelea kuhakikisha inatatua changamoto zinazolikabili kundi hilo ikiwemo magonjwa ya kuambukiza,ukatili wa kijinsia , ndoa za utotoni na mimba mashuleni ili watoto wa kike waweze kufikia malengo yao.

Majaliwa ameyasema hayo leo April 17 Jijini hapa wakati wa uzinduzi huo ambapo aliwataja Vijana kuwa ni kundi kubwa hivyo kuna umuhimu wakuliangalia kwa ukaribu.

Akizindua ajenda hiyo ya Kitaifa,alibainisha kuwa Lengo la ajenda hiyo ni kuwekeza katika Sekta hiyo na maendeleo kwa vijana hasa kwa kuondoa vikwazo kwa vijana,kuongeza kasi ili kuleta mabadiliko kwa jamii.

“Serikali imeweka bayana kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kupitia ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutaka vijana kuhamasishwa kupima afya zao,nichukue nafasi hii Kutoa wito kwa jamii kuondoa ushawishi wa ngono kwa watoto wa kike ili waweze kumaliza masomo yao,”amesema

Licha ya hayo alizitaja nguzo za kuzingatia Katika kundi balehe kuwa ni mapambano dhidi ya Ukimwi,ukatili wa kijnsia,lishe,kupinga mimba za utotoni,kuwasimamia wanafunzi kumaliza shule na kuwajengea vijana balehe ujuzi na uwezo wa kuzifikia fursa mbalimbali za kiuchumi.

Awali akitoa maelezo kuhusiana na Ajenda hiyo ya Kitaifa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa chimbuko la ajenda hiyo na lengo lake imetokana na tafiti mbalimbali nchini ambazo zilionyesha ongezeko la vijana balehe wanao ambukizwa virusi vya ukimwi na utatuzi wa changamoto hizo.

Amesema matarajio ya Wizara hiyo ni kuona vijana wote kwenye jamii wanakuwa salama na kwa wale ambao tayari wamepata maambukizi ya Ukimwi wanapata huduma nanushauri nasaha.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Wizara yake itaimarisha mitaala shule za msingi na vyuo ili kuibua Ubunifu na kuongeza fursa za elimu Katika ufundishaji.

Kwa upande wake Balozi wa uwasilishwaji wa nguzo kuu sita za vijana balehe,Nzengo Nsomi alitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za ukimwi kwa vijana balehe ikiwa ni Pamoja na kuwafundisha mbinu sahihi za kujikingà ili kuwanusuru vijana na Kuwa na Taifa salama .

“Nguzo namba moja kwa vijana balehe ni mapambano dhidi ya ukimwi,vijana balehe Wenye umri Kati ya miaka 10-19 bado tupo hatarini ,tunaomba serikali kuongeza nguvu zaidi Katika mapambano,”amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles