25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Kizimbani kwa kumlawiti mtoto wake mwenye miaka sita

Omary Mlekwa -Hai

MFANYABIASHARA  wa wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni mkazi wa Bomang’ombe,  Ramadhani Tesha (44),  amefikishwa katika  Mahakama yaHakimu Mfawidhi ya Wilaya hiyo akikabiliwa  na shitaka la  kumlawati mtoto wake mwenye umri wa  miaka sita.

 Akisoma hati ya  mashitaka, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Lobulu Mbise, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Devota Msofe,  alidaiwa mshitakiwa anakabiliwa na shitaka la kumlati mtoto wake anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kingereka wilayani humo  uku akitambua kufanya hivyo ni kosa.

Mbise alidai Januar 23 mwaka  kwa nyakati tofauti katika eneo la Kibaoni Bomang’ombe, mtuhumiwa alimfanyia ukatili huo mtoto wake kinyume na kifungu 154 (11) (a) (2) cha sheria ya adhabu  sura 16 kama iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka lake na mahakama kushindwa  kutoa dhamana kwa mshitakiwa  kwa kohofia  usalama wake kutokana na jamii inayomzunguka kuhofiwa kumdhuru kutokana na na tukio hilo.

“Kesi hii ninaiharisha hadi Februari 13 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na mtuhumiwa utakwenda magereza hadi hiyo siku kutokana na hali ya usalama wako kwenye jamii” alisema hakimu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles