25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kukutwa na bangi

ERICK MUGISHA-DAR ES SALAAM

Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Tabata Mtambani, Novati Valentino (22) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kukutwa na Madawa ya kulevya aina ya Bangi. 

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Hilda Katu amemsomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Irene Lyatuu na kudai Septemba 11 mwaka huu katika eneo la Kigogo Wilayani Ubungojijini Dar es salaam alikutwa na madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa gramu 92.67.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama na mwendesha mashtaka wa jamuhuri akidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kuomba mahakama kutoa tarehe nyingine.

Hakimu Lyatuu amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wanaofanya kazi kutoka taasisi inayotambulika kisheria,  barua kutoka kwa waajiri wao, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya sh 1,000,000 kwa kila mdhamini. 

Hata hivyo mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itakuja kutajwa tena Desemba 30 mwaka huu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles