26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa dawa za kulevya, bangi

NA WAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imempandisha kizimbani mkazi wa Manzese, Michael Nikolai (25) kwa tuhuma ya kukamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 15.89.

Awali, akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Denis Mlashani, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Chesence Gavyole, alidai mnamo Julai 4 mwaka huu katika eneo la Manzese Sokoni, mtuhumiwa alikamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume cha sheria 17(1), (2) cha sheria ya kudhibiti dawa za kulevya.

Hata hivyo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa huku upande wa jamhuri ulidai upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mlashani alisema kesi hiyo inadhaminika endapo mtuhumiwa atakidhi vigezo vya dhamana vya kuwa na wadhamini wawili waaminifu.

Aidha wawe wafanyakazi wa Serikali wenye barua za utambulisho kutoka Serikali zao za mitaa na vitambulisho vya taifa.

Mtuhumiwa alishindwa kukidhi vigezo vya dhamana kwa kutokuwa na wadhamini, hivyo alirudishwa rumande hadi Oktoba 12. 

Wakati huo huo, Mkazi wa Tandale, Robert Vicent (36), mfanyabiashara, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la kuharibu mali kwa makusudi.

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Hudi Majid Hudi, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Madarakini Emmanuel, alidai mnamo Septemba 9, 2019 mshtakiwa aliharibu kompyuta yenye thamani ya Sh 1,750,000.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo mbele ya hakimu Hudi, huku upande wa jamhuri ukidai upelelezi umekamilika.

Hakimu Hudi alisema kesi hiyo ina dhamana endapo mshtakiwa atakidhi vigezo vya dhamana, vya kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaosaini mkataba na mahakama wa Sh 1,000,000 pia wenye barua za utambulisho kutoka Serikali za mitaa.

Mshtakiwa huyo alikidhi vigezo vya kuwa na wadhamini wawili, huku Hakimu Hudi alisema shauri hilo litatajwa tena Oktoba 10, mwaka huu.

Habari hii imeandikwa na GODFREY SHAURI, YUSUPH KANGABYA, WARDA LUPENZA (TUDARco) na SARAPHINA SENARA (UoI)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles