28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kimbunga Freddy; Tanzania yaipiga tafu Malawi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi Msaidizi  anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameongoza ujumbe wa kutoka Tanzania kupeleka misaada ya unga, mahindi, mablanketi, mahema na madawa mbalimbali ambayo yatasaidia wahanga wa Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela, Godfrey Kawacha akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Karonga Nchini Malawi Mhe. Roderick Mateauma (Kulia) kabla ya magari yaliobeba misaada ya Kibinadamu ya kuvuka Mpaka wa Kasumulu kuelekea Mjini Blantyre, Malawi.

Luteni Kanali Masalamado amesema hayo wakati msafara wa magari ya jeshi la Wanachi wa Tanzania yakivuka mpaka wa Kasumulu Wilaya ya Kyela kuelekea Mji wa Blantyre nchini Malawi Machi 22, 2023.

“Natoa pole kwa ndugu zetu, wananchi wa Malawi tuko nao katika hali hii ngumu,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi hicho Luteni Kanali George Kamya amesema wanasikitika kwa yale yaliyotokea nchini Malawi baada ya kupigwa na Kimbunga Freddy.

“Katika kuitikia hilo serikali ya Tanzania imetoa msaada kuwasaidia wenzetu waliopata na haya Majanga,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karonga nchini Malawi, Roderick Mateauma ameishukuruSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kwamba msaada huo utasaidia kupunguza athari kwa wahanga na inaonesha mahusiano ya karibu yalipo kati ya nchi hizo mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles