26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

KILIMO CHA MKATABA KUONGEZA UZALISHAJI PAMBA

Na MWANDISHI WETU-MWANZA

WAKULIMA wa pamba nchini, wamehimizwa kujiunga na kilimo cha mkataba kwa kuwa kina faida na mafanikio kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), James Shimba, alisema kilimo cha mkataba kimesaidia kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba na matumizi ya mbegu bora aina ya UK M08.

Pia, alisema kilimo hicho kimesaidia katika usambazaji na matumizi ya viuadudu na upatikanaji wa huduma za ugani.

“Kilimo cha mkataba kimewafanya wakulima wa ukanda wa Magharibi unaojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Tabora, Singida, Kagera na Kigoma, kupata usimamizi mzuri wa sheria na sera za kilimo kupitia maofisa ugani walioko kwenye halmashauri zao za wilaya.

“Kilimo hicho pia kimesaidia kuongeza eneo la uzalishaji wa pamba, matumizi makubwa ya mbegu za kupanda, ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuhakikisha wakulima wengi zaidi wanajiunga na kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba.

“Kwa sasa pamoja na kwenda vizuri, kuna changamoto ambayo bodi ya pamba inaendelea kukabiliana nayo kwa kutoa elimu ya kilimo cha mkataba ambapo tunawaelimisha namna ya kulima kwa kuzingatia vipimo na maelekezo yanayopendekezwa na wataalamu.

“Tunawasisitiza sana kuacha kuchanganya pamba na mahindi na pia wasiweke maji na mchanga kwenye pamba kwani hivyo ni vikwazo vingine vya kuongezeka kwa uzalishaji.

“Lakini pia, tunawahimiza wang’oe na kuchoma moto miche ya pamba baada ya kuvuna kwa kuwa wakiiacha inakuwa mazalia ya wadudu waharibifu wa pamba.

“Katika kilimo hiki, wakulima wanapaswa kutambua kuwa tija katika kilimo cha pamba ikiogezeka mara dufu, kipato cha mkulima pia kitaongezeka.

“Hivyo basi, lazima iwepo mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji kwa kushirikiana na wakulima, wachambuaji wa pamba, viongozi wa ngazi ya wilaya na Serikali Kuu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Mimi ninawazo tofauti na mpango wa bodi ya pamba na nikipewa nafasi ya kusimamia kilimo cha pamba tija itaonekana haraka naomba nipewe hiyo kazi mara moja nianze utekelezaji mimi ni mtumishi wa wakulima TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles