31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

KIKWETE, LOWASSA KUMZIKA MMILIKI IMPALA HOTELS LEO

Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kuongoza mamia ya wakazi wa Arusha katika mazishi ya mfanyabiashara maarufu wa jijini hapa, Faustine Mrema aliyefariki hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Mbali na Kikwete, viongozi wengine watakaoshiriki mazishi hayo, ni mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali, wabunge na wawakilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Sekta ya Utalii.

Mrema aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita katika Hospitali ya Garden, Afrika Kusini,  anatarajiwa kuzikwa saa 8 mchana nyumbani kwake eneo la Ngurdoto.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu eneo la Sanawari Uzunguni jana, msemaji wa familia, Vincent Laswai, alisema taratibu zote za mazishi zimekamilika.

“Viongozi mbalimbali marafiki wa Mrema wamethibitisha kushiriki mazishi, wataongozwa na Kikwete ambaye yuko safarini Nigeria, lakini amesema atawahi mazishi, wapo pia Lowassa na Sumaye.

“Pia tunatarajia uwakilishi mkubwa kutoka serikalini, viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wafanyakazi na wanajumuiya ya Impala na watu kutoka maeneo mabalimbali, kwa hivyo mtaona jinsi tunavyotarajia kupata ugeni mkubwa,” alisema Laswai.

Alisema mwili wa marehemu unatarajiwa kuondolewa nyumbani kwake eneo la Sanawari saa 2 asubuhi kuelekea Ngurdoto na kutanguliwa na ibada ya mazishi.

Wakati wa uhai wake, Mrema alikuwa akimiliki biashara mbalimbali, hasa kwenye sekta ya utalii, zikiwamo  hoteli za kitalii za Ngurdoto Mountain Lodge, Impala Hotel Arusha na Moshi, Naura Springs, kampuni za utalii za Classic Tours na Impala Shuttle.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles