26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA BOSI JAMII FORUMS KUANZA KUSIKILIZWA

NA KULWA MZEE

-DAR ES SALAAM

KESI inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake, inatarajia kuanza kusikilizwa Agosti 24, mwaka huu.

Melo na mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forums, Micke William, wamesomewa maelezo ya awali kwa kesi inayowakabili ya kuzuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa, juzi aliwasomea maelezo ya awali washtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa.

Washtakiwa walikubali maelezo yao binafsi na kukana shtaka linalowakabili.

Inadaiwa katika maelezo ya awali kwamba Melo na William ni wamiliki na waanzilishi wa Mtandao wa Jamii Media Co. Ltd ambao umesajiliwa Brela Julai 2, 2008 na kupewa namba ya usajili 66333.

Mutalemwa alidai kuwa katika uendeshaji wa mtandao, ili mtu aweze kuutumia ni lazima asajiliwe kwa kutoa majina yake, anuani na namba ya simu.

Alidai baada ya usajili, hupatiwa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika, hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo wa kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Mutalemwa alidai kuwa Mei 10, 2016, Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), aliwaandika barua washtakiwa, akiwafahamisha ofisi yake inafanya upelelezi juu ya taarifa ya uongo dhidi ya Cusna Investment na Ocean Link iliyochapishwa na mwanachama wao, Kwayu JF senior Expert Member na Amrishipuri.

Alidai aliwafahamisha kwa kifupi taarifa ambayo anaihitaji kutoka kwao na maelezo binafsi ya mtu aliyechapisha ili aweze kufanya upelelezi.

Mei 11, mwaka jana, inadaiwa mfanyakazi wa Jamii Media, Chrispin Mganyizi aliipokea taarifa na kuiwasilisha kwa washtakiwa, lakini walikwamisha polisi kufanya upelelezi kwa kuficha taarifa za wanachama wao, Kwayu JF senior Expert Member na Amrishipuri.

Micke na Melo katika kesi hiyo,wanadaiwa kati ya Mei 10 na Desemba 13, 2016 , Mikocheni, Dar es Salaam wakiwa wakurugenzi wa taasisi hiyo, wakijua Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuhusu mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yao, kwa njia ya kuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa data walizonazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles