22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MPANGO AWATOLEA UVUVI WATUMISHI

Na Mwandishi Wetu

-LINDI

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amewataka watumishi wa wizara na taasisi zilizo chini yake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na Serikali yao.

Kauli hiyo aliitoa jana alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonesho Nanenane katika eneo la Ngongo Mkoani Lindi.

Alisema kuwa Wizara hiyo inategemewa na wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuripamoja na kutoa elimu kwa umma vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.

“Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia,” alisema Dk. Mpango.

Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu ambayo ni ya 24 kufanyika  ni Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles