27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WENYEVITI CUF WAMUUNGA MKONO PROF. LIPUMBA

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

SIKU chache baada ya Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) chini ya mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama wabunge wanane wa viti maalumu, wenyeviti wa Serikali za mitaa 70 wameunga mkono uamuzi huo.

Wenyeviti hao pia  wamepinga taarifa iliyotolewa  na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Mzimuni, Bakari Kasubi   mwezi uliopita   kumuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na Baraza Kuu lake katika mgogoro unaoendelea   ndani ya chama hicho.

Wenyeviti wa mitaa 14 waliofuatana  na wajumbe wao wa mitaa mbalimbali walitoa tamko hilo   Dar es Salaam jana kwa niaba ya wenzao 36 katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho  Buguruni, wilayani Ilala.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga ‘B’,  Shilingi Shilingi, alisema wanaunga mkono uamuzi uliofanywa hivi karibuni na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho la kuwavua uanachama wabunge ambao ambao walikuwa wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume cha nidhamu ya chama hicho.

Alisema licha ya uamuzi huo,    wanamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu aliyeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF na nafasi yake kukaimiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya.

“Uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ni sahihi, la kuwavua unachama wabunge wanane na madiwani wawili ambao vitendo vyao vilikuwa ni hujuma ya wazi kwa chama chetu.

“Ni lazima wajue kwamba CUF ipo imara si kwa hawa tu hata  wengine wakijitokeza kukihujumu chama wachukuliwe hatua. Wale wote wanaoingilia mgogoro huu bila kujua undani wake waache mara moja,” alisema Shilingi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bwawani, Mohamed Mkandu alitaja sababu mbalimbali zilizowafanya waamue kumuunga mkono Profesa Lipumba na Baraza Kuu la Uongozi lililochukua uamuzi huo.

Alizitaja sababu hizo kuwa ni kuwa wanamtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti halali wa CUF licha ya hatua yake ya kujiuzulu kabla ya kurudi ndani chama hicho kwa sababu  hakurudi kwa utashi wake ila ni uamuzi wa  katiba.

Mkandu ambaye pia Katibu wa CUF Wilaya ya Kinondoni, alisema   wanamuunga mkono mwenyekiti huyo ambaye amekijenga chama hicho kwa gharama kubwa ikiwamo kupata misukosuko ya kutiwa mbaroni na vyombo vya dola mwaka 2001.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles