25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Kiiza mchezaji bora Simba

KIIZANA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamis Kiiza ‘Diego’, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba wa timu hiyo, iliyotolewa kabla ya kuanza kwa mazoezi yao Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana.

Kiiza amepewa zawadi ya tuzo yenye picha ya kiatu pamoja na mpira na kiasi cha fedha cha Sh 500,000, akiwapiku wachezaji wenzake ambao nao walikuwa wakiishindania. Tuzo hiyo ya Kiiza imetokana na moto wake wa kufunga mabao Ligi Kuu akiwa kileleni amefunga matano yaliyoifanya timu yake kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa kujikusanyia pointi 12.

Mganda huyo, 24, pia amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye ligi hiyo kupiga ‘hat trick’ (mabao matatu) msimu huu, aliyofunga dhidi ya Kagera Sugar walipoichapa 3-1.

Mara baada ya Kiiza kupewa tuzo hiyo, wachezaji wote wa Simba waliokuwa mazoezini walisimama kwa pamoja wakiwa na bango lililoandikwa ‘Tanzania Kwanza’ la kuhamasisha amani nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Kikosi cha Simba kinaendelea kujinoa chini ya Kocha Mkuu, Dylan Kerr, wakijiandaa na michezo miwili migumu ijayo watakayocheza jijini Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine dhidi ya Mbeya City (Oktoba 17) na Tanzania Prisons (Oktoba 21).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles