29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

KHLOE ATUMIA MIL 202/- MAANDALIZI YA MTOTO

ROS ANGELES, MAREKANI


MWANAMITINDO, Khloe Kardashian, wiki iliyopita alitumia zaidi ya dola za Marekani 90,000 sawa na (Sh milioni 202 za Tanzania), katika manunuzi ya vifaa vya mtoto wake mtarajiwa.

Khloe na mama yake, Kris Jenner, wiki iliyopita walionekana mitaa ya West Hollywood, katika duka la watoto la kifahari ambapo walitumia zaidi ya dola 90,000 kufanya manunuzi yao.

Nyota huyo wa tamthilia ya ‘Keep Up With The Kardashian’, anatarajia kujifungua mtoto wa kike Aprili mwaka huu na mpenzi wake, Tristan Thompson.

Miongoni mwa vitu vilivyonunuliwa ni pamoja na blanketi ya mtoto dola 365, jaketi 450, kitanda cha mtoto dola 10,000 na begi la begani dola 600.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles