Kesi ya kina Zitto ngoma nzito, serikali yadai Mahakama haisikilizi shauri la muswada

0
1348

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya kupinga Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa, iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na wenzake.

Hatua hiyo inatokana na waombaji hao, kuwasilisha maombi chini ya Ibara ya 30 ya Katiba ambayo inazungumzia sheria na si muswada kama walivyoainisha.

Wakili wa Serikali Mkuu, Mark Mulwambo ametoa madai hayo akiwasilisha hoja za kupinga usikilizwaji wa shauri hilo ambalo limeanza kusikilizwa leo katika mahakama hiyo.

Aidha, amedai Katiba imeipa Bunge kinga ya kutoingiliwa katika kutekeleza shughuli zake na pia inazuia mahakama kujadili muswada na mahakama inajadili sheria si muswada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here