27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Kazi imeanza vita mifuko ya plastiki

Na WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WAKATI leo ukiwa ni mwanzo wa matumizi  mbadala wa mifuko ya plastiki kama ambavyo sheria na kanuni za Usimamizi wa Mazingira za kupiga marufuku mifuko hiyo za mwaka  2019  zinavyoelekeza, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) tayari jana lilianza kazi ya kusambaza maofisa wake kwa ajili ya kukagua utekelezaji huo.

Akizungumza  jana Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema  maafisa hao  ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo viwandani  na katika maduka makubwa wamefanya kazi ya kukagua na tayari wamekuta kiwanda kimoja kikiwa na tani 100 za mifuko hiyo.

  “Nasubiri maafisa ambao walikuwa katika maeneo mbalimbali nchini kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ili niweze kutoa takwimu sahihi za shehena za mifuko ya plastiki zilizosalimishwa,” alisema Heche.

Alisema  mwitikio wa watu katika zoezi hilo ni mkubwa na  hasa katika mikoa ya Dar es Salaam  na Pwani.

“Mwitikio ni mzuri mfano Mkuranga viwanda vyote vimeshafungwa na kusitisha uzalishaji,kuna kiwanda tumekikuta na zaidi ya tani 100 na  wameshafunga,”alisema Heche.

Kupitia ukurasa wake Twitter, Waziri wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais  Mazingira na Muungano, Janaury Makamba aliandika kuwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles