29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Jua Cali huyoo kwa Snoop Dogg, Dr Dre

jua-kaliNAIROBI, KENYA

MKALI wa wimbo wa ‘Kwaheri’, Paul Nunda ‘Jua Cali’, anatarajia kusonga mbele kimataifa kutokana na mpango wake wa kufanya kazi na wasanii wakali duniani akiwemo, Snoop Dogg na Dr Dre.

Jua Cali hakutoa wimbo mpya tangu mwaka 2008 alipotoa wimbo wa ‘Kwa heri’ uliokuwa kwenye chati za juu Afrika Mashariki, lakini kwa sasa msanii huyo amewekeza muziki wake katika soko la kimataifa hasa kwa wasanii wa Marekani, Snoop na Dr. Dre.

“Ninaamini nina uwezo mkubwa kwa kuwa nilifanya vizuri miaka ya nyuma lakini nilikaa kimya kutokana na mambo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wangu, ila kwa sasa natarajia kufanya mambo makubwa ambayo sijawahi kuyafanya.

“Kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kazi na wasanii nyota wa nchini Marekani, Dr Dre na Snoop Dogg, ninaamini hii itanifanya nivuke mipaka,” alisema Jua Cali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles