27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Juliana anasa kwa Mr Flavour

ed3BoQtNAIROBI, KENYA

NYOTA wa muziki nchini Uganda, Juliana Kanyomozi, ameonekana kunasa kwenye penzi la msanii wa Nigeria, Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’, baada ya kukutana nchini Kenya katika maonyesho ya Coke Studio.

Wasanii hao wamekutana nchini humo kwa ajili ya muziki uliokutanisha wasanii mbalimbali kutoka Afrika, ambapo wanafanya muziki kwa kushirikiana, lakini ukaribu wa Mr Flavour na Juliana umewafanya mashabiki wao kudhani kuna lingine zaidi ya muziki baina yao.

Mitandao mbalimbali nchini humo inaeleza kwamba wawili hao baada ya kufanya kazi pamoja, Juliana alionekana akitumia muda mwingi akiwa karibu na msanii huyo na walionekana kuwa na ukaribu uliokuwa na uhuru wa kupitiliza.

Kupitia akaunti ya Instagram, Juliana aliweka ujumbe wa kumtakia Mr Flavour heri ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandika: “Hongera kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa, umekuwa msanii ambaye unanifanya nijisikie nipo juu kutokana na jinsi unavyonishauri, ninaamini tutaendelea kuwa pamoja, nakupenda sana.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles