Mo Music kusaka video Afrika Kusini

0
1412

Mo-musicNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII Moshi Katemi ‘Mo Music’, amepanga kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya upigaji wa picha za video ya wimbo wake mpya wa ‘Skendo’.

Video hiyo inatarajiwa kuandaliwa na mwongozaji mashuhuri nchini, Adam Juma ambaye wamepanga kwenda naye nchini humo kwa ajili ya kazi hiyo.

“Sitaki kuwaangusha mashabiki wangu, nitakwenda Afrika Kusini kufanya video ya Skendo ila nitamtumia Adam Juma kwa sababu ni mwongozaji bora na huwa tunafanya kazi nzuri kila tunapokutana,” alisema Mo Music.

Mo Music aliongeza kwamba hiyo itakuwa video yake ya tatu kufanya na mwongozaji huyo mkongwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here