Jose Chameleone ampiga chini mkewe

0
1615
Jose Chameleone na Mkewe

KAMPALA, UGANDA

HATIMAYE staa wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone, ameachana na mke wake, Daniella, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka 10.

Miezi michache iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba wawili hao wapo kwenye mgogoro na wanatarajia kuachana, huku ikidaiwa kwamba msanii huyo si mwaminifu kwa mke wake.

Mbali na suala la uaminifu, lakini inadaiwa sababu nyingine ya kuachana kwao ni pamoja mrembo huyo kuchoka kitendo cha kumpiga mara kwa mara.

Hata hivyo, Chameleone, aliamua kufunguka na kuweka wazi kuwa, anajilaumu kwa kitendo cha kuwa mwanamume bora kwa mke wake pamoja na watoto kwa ujumla.

“Kila kitu kina mwanzo na mwisho, nimeshindwa kuwa baba bora kama nilivyotakiwa kwa familia yangu, nini kinatakiwa kwa sasa ni Mungu kutujalia na ninaamini ataendelea kuwa pamoja nasi.

“Hizi ni habari za kweli na wala si kiki kama watu wanavyodhani na si kama natangaza kuwa natafuta mpenzi, kwa sasa inatosha, nimejigundua kuwa siwezi kubadilika,” alisema Chameleone.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here