28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

JKCI YAHITAJI CHUPA 300 ZA DAMU

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi

Na VERONICA ROMWALD– DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inahitaji zaidi ya chupa 300 za damu kwa wagonjwa kati ya 200 hadi 250 ambao inatarajia kuwafanyia upasuaji kati ya Novemba na Desemba, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuwezesha kufanikisha matibabu hayo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Profesa Janabi alisema wanatarajia katika kipindi hicho kupokea vikundi vitano vya wataalamu waliobobea katika kutibu magonjwa ya moyo kutoka nchi mbalimbali.

Alizitaja nchi hizo ni pamoja na India, Austraria, Dubai, Falme za Kiarabu, Ujerumani na Israel.

“Tumekusudia kabla ya kufunga mwaka 2017 tuwafanyie upasuaji wagonjwa 1,400, tutakapowafanyia upasuaji wagonjwa hawa tutakuwa tumeweza kufikia lengo letu hilo tulilojiwekea mwanzoni mwaka huu,” alibainisha.

Profesa Janabi alisema kati ya Novemba 6 hadi 10, mwaka huu wanatarajia kuwafanyia upasuaji mkubwa wa kuvuna mishipa ya damu kutoka miguuni kwenda kwenye moyo wagonjwa 15.

“Upasuaji huu kitaalamu unaitwa bypass, tutafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na wenzetu kutoka India,” alibainisha.

Profesa Janabi alisema kuanzia Novemba 6 hadi 10, mwaka huu  watafanya upasuaji kwa watu wazima ambao milango yao ya moyo imeharibika.

Alisema Novemba 3 hadi 10 watapokea pia madaktari bingwa kutoka nchini Australia ambao watawafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na magonjwa ya moyo wapatao 50.

Profesa Janabi alisema Novemba 23 hadi 27 wanatarajia kupokea vikundi vingine viwili vya madaktari bingwa kutoka Israel na Ujerumani wenye uwezo wa kuwafanyia upasuaji hadi watoto wachanga waliozaliwa na magonjwa hayo.

“Kati ya Novemba 14 hadi 19, mwaka huu tutapokea wataalamu kutoka Dubai na tutawafanyia upasuaji wagonjwa wapatao 70 wa kutibu magonjwa ya moyo bila kufungua kifua,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles