31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Jeshi la kulinda amani lapelekwa Kinshasa

cnqbvy7xgaar3fu
Herve Ladsous

 

KINSHASA, DRC

UMOJA wa Mataifa unawahamisha mamia ya walinda amani wake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) kwenda Kinshasa.

Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limewanukuu maofisa wa umoja huo wakisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusaidia kukabiliana na uwezekano wa ghasia kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais.

Maofisa walisema kuwa takribani wanajeshi 300 na polisi kutoka kikosi cha kulinda amani nchini hapa (MONUSCO) watakuwa Kinshasa, eneo ambako ghasia zilisababisha vifo vya watu 49 mwezi uliopita.

“Tunapanga kwa hali yoyote na tumechukua hatua kuimarisha uwepo wetu Kinshasa,” alisema mkuu wa kikosi hicho, Herve Ladsous.

Hata hivyo, Ladsous ameonya kuwa huenda wanajeshi hao wanaotumwa wasitoshe iwapo mji mkuu huo utashuhudia ghasia kubwa zaidi.

“Ni muhimu tukumbuke kuwa Kinshasa ni mji wa takribani watu milioni 11 na MONUSCO haina idadi ya kutosha ya wanajeshi,” alisema.

Wasiwasi wa kisiasa umeongezeka katika kinachoonekana kuwa jitihada za Rais Joseph Kabila kusalia madarakani.

Hata hivyo, makubaliano yalifikiwa wiki hii kusogeza mbele uchaguzi wa rais hadi Aprili 2018.

Lakini upinzani umesusia makubaliano hayo na kutishia kufanya maandamano makubwa jana.

Kutokana na wito huo wa upinzani, biashara zilifungwa mjini hapa jana na hakukuwa na magari barabarani.

Vikosi vya usalama vimeizingira nyumba ya mpinzani mkuu wa Kabila, Etienne Tshisekedi, anayeongoza wito wa uchaguzi ufanyike Novemba mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles